Siku Za Kupata Mimba

Siku Za Kupata Mimba

(Siku ya Ovulation/kuanguliwa kwa yai)

Ndiyo kipindi ambapo yai lililokomaa hutolewa na ovari na kuanza kusafiri kuelekea kwenye mfuko wa uzazi kupitia mirija ya uzazi (falopian tubes).

Ikitokea limekutana na mbegu ya kiume likiwa bado lipo ndani ya mirija hii ya uzazi (ndani ya masaa 24 tangu litolewe) basi mimba hutungwa.

Hapa chini nimekupa utaratibu wa lini hasa siku hii hutokea kwa mizunguko yote ya hedhi pamoja na siku zake za hatari.

1)Mzunguko wa siku 22,hutokea siku ya 8 ya mzunguko huku siku za hatari zaidi ni siku ya 6-9

2)Mzunguko wa siku 23,hutokea siku ya 9 na siku za hatari zaidi ni 7-10

3)Mzunguko wa siku 24,hutokea siku ya 10 na siku za hatari zaidi ni 8-11

4)Mzunguko wa siku 25,ni siku ya 11 huku siku za hatari zaidi ni 9-12

5)Mzunguko wa siku 26,ni siku ya 12 huku siku za hatari zaidi ni 10-13

6)Mzunguko wa siku 27 hutokea siku ya 13,siku za hatari zaidi ni 11-14

7)Mzunguko wa siku 28 hutokea siku ya 14,siku za hatari zaidi ni 12-15

8)Mzunguko wa siku 29 ni siku ya 15,siku za hatari zaidi ni 13-16

9)Mzunguko wa siku 30 ni siku ya 16,siku za hatari zaidi ni 14-17

10)Mzunguko wa siku 31 ni siku ya 17,siku za hatari zaidi ni siku ya 15-18

11)Mzunguko wa sku 32 ni siku ya 18,siku za hatari zaidi ni 16-19

12)Mzunguko wa siku 33 ni siku ya 19,siku za hatari zaidi ni 17-20

13)Mzunguko wa siku 34 ni siku ya 20,siku za hatari zaidi ni 18-21

14)Mzunguko wa siku 35 ni siku ya 21,siku hatari zaidi ni siku ya 19-22

15)Mzunguko wa siku 36 ni siku ya 22,siku za hatari zaidi ni 20-23

NAMNA YA KUHESABU.

Mizunguko hii huwa tunahesabu kuanzia siku ya kwanza ya hedhi(siku ya kwanza damu na uchafu kuanza kutoka) hadi siku moja kabla ya kuanza tena kwa mwezi mwingine.

Mfano,ikiwa hedhi imeanza leo basi siku hii ni ya kwanza,endelea kuhesabu siku hizi hadi siku moja kabla haijaanza tena kwa mwezi mwingine.

TU FOLLOW KATIKA MITANDAO YA KIJAMII