Vidonda Vya Tumbo

Vidonda Vya Tumbo.

Vidonda vya tumbo ni matokeo ya kuharibika kwa uteute wa ndani ya ukuta wa tumbo la Chakula au ndani ya utumbo mdogo wa Chakula na matokeo yake ni ukuta wa tumbo kugusana na tindikali iliyoko tumboni ambayo ni kali sana.

NINI HUSABABISHA

vidonda vya tumbo husababishwa na maambukizi ya bacteria waitwao HELICOBACTER PYLORI, aidha matumizi ya baadhi ya dawa za kutuliza maumivu za jamii ya Nonsteroids anti inflammatory drugs kama vile ASPIRIN /DICLOFENAC huweza kusababisha uwezekano wa kupata ugonjwa huu,

Vidonda vya tumbo vinaweza kujitokeza katika utumbo mdogo na katika tumbo la Chakula na pia ni Mara chache huweza kujitokeza katika koo la Chakula ambapo hapakukusudiwa kustahimili tindikali ya tumbo.

Kuna Aina tatu za Vidonda vya Tumbo(peptic ulcers).

1.GASTRIC ULCERS.

Hivi ni vidonda vinavyotokea katika mfumo wa Chakula yani tumboni.

2.DUODENAL ULCERS.

Hivi ni vidonda vinavyotokea katika utumbo mdogo.

3.OESOPHAGEALS ULCERS.

Hivi ni vidonda vinavyotokea katika koo/koromeo la Chakula

Kila aina ya vidonda vina Hatua nne.

HATUA YA KWANZA:

Hatua ya kwanza ya huu ugonjwa ni ule uvimbe sugu unaotokea sehemu ya ndani ya tumbo.

HATUA YA PILI.

Hapa vijidonda hujitokeza sehemu zenye uvimbe na taratibu vidonda hivyo huongezeka na kua vikubwa katika hatua hii mgonjwa hupatwa na maumivu makali ya tumbo yanayodumu kwa muda mrefu yakiambatana na kiungulia,tumbo kujaa gesi wakati wote,kukosa hamu ya kula,choo kuwa kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu,hata hvyo Hali hii ya kukosa choo kwa muda mrefu (CHRONIC DYSPEPSIA) yani kushindwa kufanya Kazi kwa mfumo wa mmeng’enyo wa Chakula kutokana na tindikali nyingi inayozalishwa tumboni huingia Kwenye mzunguko wa damu hivyo mgonjwa hujisikia uchovu na kizunguzungu cha Mara kwa Mara katika hatua hii tindikali husababisha magonjwa ya ini na Figo kwa kuwa tayar iko katika mfumo mzima wa damu

HATUA YA TATU.

Hii ni hatua ambayo ni ya hatari kwasababu vidonda vikubwa hupasua mishipa yote midogomidogo ya damu na kusababisha damu kuvia tumboni na kubadilisha rangi ya choo kuwa ya kawaida,pia damu nyingi ikivujia tumboni mgonjwa hutapika na kuharisha damu Hali hii husababisha mgonjwa kuishiwa damu Mara kwa Mara,maumivu makali ya tumbo,hupata Homa,
maumivu ya viungo na kukosa hamu ya kula.

HATUA YA NNE.

katika hatua hii ya nne saratani ya utumbo inahusika kwani katika hatua hii vidonda vya tumbo hutengeneza tundu katika tumbo au utumbo mdogo na kusababisha kuoza kwa viungo vya ndani na matokeo yake ni saratani ya utumbo

KWA KIFUPI

Seli ndani ya mwili lazima zibaki katika kiasi kidogo cha alkalini kutoka 7.2 mpaka 7.4, wakati 7.0 ni ya kati au husemwa sifuri katika kipimo cha PH yaani potential hydrogen.

Chini ya 7.0 ni asidi na juu ya 7.0 ni alkalini.

Unaweza kukinunua kipimo cha PH na kupima Ph ya mate yako au ya mkojo wako kila mara ili kupata mwelekeo wa namna gani ufanye alkalini katika mwili wako ibaki kuwa ya 7.2 mpaka 7.4 kwenye seli ndani ya mwili wako.

Ikiwa mate yanasoma 6.0 au 6.5 ni kiashiria kuwa una asidi iliyozidi kwenye seli zako.

Kila mtu anapaswa kula zaidi vyakula vyenye alkalini yaani matunda na mboga za majani na kunywa vinywaji vyenye asidi chache na ikibidi basi atumie vinywaji vyenye alkalini nyingi kama juisi ya limau,juisi ya chungwa,ya zabibu na maji halisi.

Kwa maneno mengine,hali ya uasidi ndani ya mwili ndiyo hupelekea kusikia maumivu yatokanayo na vidonda vya tumbo.

Tafiti zinaonyesha takribani mtu mmoja katika kila watu wanne anasumbuliwa na vidonda vya tumbo.

Dalili za vidonda.

👉Kuchoka choka sana bila sababu maalumu.

👉Kuuma mgongo au kiuno.

👉Kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu za kijinsia.

👉Kizunguzungu.

👉Kukosa usingizi au usingizi wa mara kwa mara.

Maumivu makali ya mwili.

👉Kifua kwa ndani kana kwamba unachomwa na kitu cha moto au chenye ncha kali.

👉Maumivu wakati mwingine hutokeza mgongoni na huchoma kama sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali.

👉Kichefuchefu.

👉kiungulia.

👉tumbo kujaa gesi.

👉tumbo kuwaka moto.

👉maumivu makali sehemu kilipo kidonda.

👉Kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu au chenye kukatika kama cha mbuzi.

👉Kutapika nyongo.

👉Kutapika damu au kuharisha damu.

👉Sehemu za mwili kupata ganzi.

👉Kukosa hamu ya kula.

👉Kula kupita kiasi.

👉kusahahu sahau na hasira za haraka.

Ni vigumu sana kueleza maumivu yote apatayo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hasa kwa mwenye vidonda sugu kwani hakuna hata kiungo kimoja mwilini atakachokuambia ni kizima.

Vitu vinavyohusika katika kuleta vidonda vya tumbo.

Asidi iliyozidi mwilini.

Unapokaribia kutaka kula chakula chochote,au ukiwaza kutaka kula au ukiona tu chakula kwa macho, TUMBONI MWAKO HUZARISHWA haidrokloriki asidi ili kuuandaa na kuusaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula,Kadri unavyoendelea kuishi haidrokloriki ASIDI HIYO HUENDA KUTOBOA KUTA ZA TUMBO na hatimaye taratibu baadaye hukusababishia vidonda.

Utokeaji wa vidonda vya tumbo hutegemea zaidi juu ya vipengele viwili

1.Vitu ambavyo huongeza mnyunyizo wa asidi katika tumbo, ikiwemo.

-vyakula vya kusisimua,
-vyakula vya mafuta,
-uvutaji wa sigara,
-utumiaji pombe,
-chai,
-kahawa,
-baadhi ya dawa tunazotumia kujitibu maradhi mbalimbali mwilini, n.k.

2.Mfadhaiko au msongo wa mawazo.

Mfadhaiko/msongo wa mawazo utokanao na maisha ni moja ya vipengele vikuu vinavyosababisha vidonda vya tumbo.

Mfadhaiko/msongo huongeza utiririkaji wa asidi ndani ya tumbo.

Hii asidi ya ziada ambayo hutiririka ndani ya tumbo kama matokeo ya mfadhaiko/msongo na hakuna chakula cha kufanyiwa kazi au kumeng’enywa humomonyoa kuta za tumbo na hivyo kusababisha vidonda.

Utafiti unaonyesha kuwa akili hutumia sehemu kubwa ya nguvu ya mwili.

Mfadhaiko/msongo huchangia sana katika kutokea kwa magonjwa mengi mwilini zaidi ya 50.

Kadiri mfadhaiko/msongo unavyokuwa ni wa muda mfupi, ndivyo pia athari zake zinavyokuwa ni fupi.

Lakini pindi mfadhaiko/msongo unapodumu kwa muda mrefu kama vile kipindi cha ndoa isiyo na amani au katika hali ya matatizo mengi yakimaisha kila mara,athari zake nazo hudumu kwa muda mrefu.

Utajuaje kama wewe ni mtu mwenye mfadhaiko/msongo,dalili zake hizi hapa.

1.Kujisikia huzuni sana kiwango cha kutokuwa na matumaini yoyote.

2.kupoteza kabisa uwezo wa akili kufurahi.

3.kupoteza kabisa hamu ya tendo la ndoa.

4.Kupoteza hamu ya chakula.

5.Kukosa usingizi.

6.Wasiwasi unaosababisha hali ya kutotulia {mpapatiko}.

7.Kupoteza kumbukumbu au hali ya kusahausahau na kushindwa kuamua.

8.Kughadhibishwa na vitu vidogo vidogo yani kitu kidogo tu unachukia mpaka mapigo ya moyo yanabadilika.

9.Kujiona huna thamani na kujitenga na marafiki hata ndugu.

Sababu nyingine inayoweza ikasababisha vidonda vya tumbo ni Haraka haraka

Maisha ya kisasa yanataka haraka katika kazi nyingi tuzifanyazo kila siku,ni lazima tufike mahala haraka na turudi haraka! Haraka hizi husababisha vidonda vya tumbo.

Atakuja mgonjwa hospital utamskia Dr “Tumbo langu linanisokota na kuniletea matatizo,au nasikia kiungulia baada ya kula”.Haraka haraka na wasiwasi ni baadhi ya sababu ya tatizo hilo.

Ili kuepuka kufanya kazi zako kwa hali ya uharakaharaka unashauriwa kupanga kabla ni kazi gani na gani utaenda kuzifanya siku inayofuatia.

Muhimu ni wewe kuwa mtu wa kiasi kwa kila jambo kwani si lazima umalize kazi zote leo.

Sababu nyingine ni ulaji wa Vyakula vya kusisimua.

Vyakula vya kusisimua ni hatari kwa neva za tumbo.

Vyakula vya kusisimua kama vile ketchup,chill sauce,achali,pilipili na vingine vingi vya jamii hii huchangia kwa kiwango fulani kudhuru neva za tumbo na havitakiwi kuliwa hasa kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na mwenye tatizo la kutosagika chakula tumboni.

Sababu ni kuwa,visisimuaji hivi huzichoma pia kuta za tumbo.

Sababu nyingine ni vyakula vyenye kaffeina na asidi nyingi

Vinywaji vyenye kaffeina na asidi nyingi kama vile chai ya rangi, kahawa,soya sauce,mayonnaise, jibini,Vyakula jamii ya Mkate,samaki wa kwenye makopo,pombe,soda na juisi za viwandani pia huchangia kwa kiasi kikubwa katika kutokea kwa vidonda vya tumbo.

NENDA KAPIME.

ili kubainisha vidonda vya tumbo nenda hospitalini utafanyiwa mionzi au X-Ray au Upimaji wa tumbo na vilivyomo ndani yake unaweza pia kufanywa na njia inayojulikana kama ‘endoskopi’ au ‘biopsi’, ambayo huyakinisha hali halisi.

VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA ILI UPONE VIDONDA VYA TUMBO.

Katika kutibu vidonda vya tumbo, mara nyingi ni lazima kupunguza uzalishaji wa asidi tumboni au mwilini kwa ujumla.

Matibabu ya vidonda vya tumbo hujumuisha lishe na kubadilisha mitindo ya maisha na kutumia dawa maalumu.

Vidonda vya tumbo endapo vipo katika hatua za awali hupona ndani ya wiki 4 mpaka 6 za matibabu.

Pia unashauriwa kufanya yafuatayo katika kujitibu au kujikinga na vidonda vya tumbo:

1.Punguza haidrokloriki asidi.(must be neutralized)kabla hujameza chakula.

INAPUNGUZWAJE.

Kwa kunywa maji kikombe kimoja au viwili nusu saa au dk 45 kabla ya kula chakula.

2.Pata usingizi wa kutosha.

Ukosefu wa usingizi ni maradhi makubwa.
Kulala ni muda ambao metaboliki ya mwili hufanyika polepole kiasi kwamba sehemu kubwa ya vyanzo vyake vya nishati hupatikana kwa ajili ya makuzi ya afya njema ya mwili na akili.
Kiwango cha wastani cha kulala kinachotakiwa hutegemeana na umri.

Katika umri wa miaka miwili, mtu hushauriwa kulala masaa 14 hadi 16 kwa siku.

Miaka 4 masaa 12 hadi 14 kwa siku.

Miaka 6 hadi 8 masaa 11 hadi 12 kwa siku.

Miaka 8 hadi 11 masaa 10 hadi 11 kwa siku.

Miaka 14 hadi 18 masaa 8 hadi 9 kwa siku.

Watu wazima wanahitaji saa za kulala kati ya 6 na 8 kwa siku.

NAMNA YAKUZIBITI MSONGO/MFADHAIKO.

Tambuwa kuwa kila mtu ana matatizo na kila mtu hufeli katika mipango yake na kila mtu hupata hasara.

Ridhika na maisha yapokee maisha kama yanavyokuja.

Karibu asilimia 50 ya wafanyabiashara wote duniani wanasumbuliwa na maradhi ya kutoridhika.kufunga choo,vidonda vya tumbo na maradhi ya moyo.

Na wafanyabiashara ambao hawajui namna ya kupambana na wasiwasi au mashaka hufa wakiwa vijana.

Punguza au acha kabisa vinywaji na vyakula vifuatavyo.

-Chai ya rangi,
-kahawa,
-pombe,
-soda,
-juisi za viwandani,
-Sigara na tumbaku zote,
-Kama wewe ni mpenzi wa kunywa chai asubuhi au jioni basi sijasema usinywe chai,bali unachotakiwa kufanya ni kuchemsha maji yako ya chai na uiunge na ama tangawizi,
mdalasini,mchaimchai,na uendelee na chai yako.

kumbuka kinachoepukwa hapa ni yale majani meusi ya chai ambayo ndani yake huwa na kaffeina na asidi nyingi na hivyo kuwa chanzo cha vidonda vya tumbo.Lakini pia tambua kuwa tangawizi peke yake ni dawa ya zaidi ya magonjwa 70 mwilini,hivyo unapokunywa chai ya tangawizi faida nyingine unayopata zaidi ya kuondoa njaa au kushiba ni dawa iliyomo ndani yake, hivyo unashiba huku unajitibu,

TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO.

Kumbuka usitumie dawa yoyote bila uangalizi wa karibu wa daktar

1.UNGA WA MAJANI YA MLONGE

Chukua kijiko kimoja sa izi ya kijiko cha chakula changanya kwenye bakuli ya mboga unapokula chakula cha mchana na jioni.

Unaweza pia kunywa unga huu wa mlonge pamoja na juisi au unaweza kuuchanganya kwenye chakula kama vile wali na hivyo ukajiongezea kinga zako dhidi ya vidonda vya tumbo.

2.KABEJI.

Kata kabeji nzima mara mbili na uchukuwe nusu yake,chukuwa karoti mbili na ukatekate vipande vidogo vidogo na utumbukize vyote kabeji na karoti kwenye blenda na uvisage ili kupata juisi yake.

Kunywa kikombe kimoja cha juisi hii kila nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi,mchana na jioni na kikombe kimoja kabla hujaingia kulala.

Rudia zoezi hili kila siku kwa wiki kadhaa na hakikisha unatumia juisi freshi pekee na siyo ukanunue juisi ya kabeji au ya karoti ya dukani.

3.UWATU.

Chemsha mbegu za uwatu kijiko kidogo cha chai ndani ya vikombe viwili vya maji,chuja na uongeze asali kidogo na unywe kwa pamoja kutwa mara 2 kwa wiki 2 au zaidi.

Unaweza pia kutumia kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa mbegu za uwatu na asali vijiko viwili vikubwa.

Au unaweza kuchemsha kikombe kimoja cha majani freshi ya uwatu, ongeza asali kidogo na unywe mara 2 kwa siku kwa wiki 2 au zaidi.

4.ASALI MBICHI.

Lamba vijiko vikubwa viwili kutwa mara tatu au vijiko vikubwa vitatu kutwa mara mbili.Fanya hivi kwa wiki 3 hadi 4.Hakikisha unapata asali mbichi salama ambayo haijachakachuliwa.

5.MAFUTA YA HABBAT SODA.

Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa hadi siku 60 hasa habbat soda grade 1.

Vidonda vya tumbo pia upate unga wa asili wa majani ya mlonge na mbegu za maboga kwa matokeo mazuri.

Kumbuka pia kunywa maji mengi ya kutosha kila siku,Epuka pia vinywaji na vyakula vyenye asidi nyingi.

Kwa tiba zilizoandaliwa kitaalam,

Wasiliana na Doctor Seifu

0679919692 / 0763311841

TU FOLLOW KATIKA MITANDAO YA KIJAMII