Faida Ya Juice Za Matunda kiafya

Faida Ya Juice Za Matunda kiafya

JUISI YA MCHANGANYIKO WA NDIZI NA CHUNGWA:
Chukua ndizi kama mbili au zinazotosha kutengenezea kiasi cha juisi upendacho na chungwa au machungwa. Kisha osha vizuri matunda yako na menya ndizi halafu zikate vipande vidogo.

Ndizi ninazozungumzia hapa ni ndizi mbivu na si vinginevyo. Weka vipande vya ndizi zako kwenye blenda kisha saga upate juisi yako.

Chukua chungwa au machungwa na kamua ili upate juisi yake kisha changanya na saga
kwa pamoja ili upate mchanganyiko ulio sahihi.
Chukua maji safi na salama kama glasi moja kisha changanya.

Unaweza kuweka sukari au asali kidogo ili kuleta ladha.
Unaweza kuweka mchanganyiko wa juisi yako kwenye friji ili ipate ubaridi kidogo na iwe tayari kwa matumizi.

FAIDA ZA JUISI HII KIAFYA:
Kumbuka tunda la ndizi lina madini ya potasiam na sodiam kidogo. Madini haya yana vitamini B na pia kuna magneziam 
ndani yake.
Virutubisho vilivyomo vinasaidia

mzunguko wa damu kwenye arteri kuwa mzuri. Pia katika mchanganyiko huu wa juisi kuna vitamini C na A.

Aidha juisi hii inasaidia kutunza na kuufanya moyo ufanye kazi yake vizuri na ina uwezo wa kuzuia shinikizo la damu (High Blood Pressure). JUISI YA MCHANGANYIKO WA APPLE NA PARACHICHI:
Chukua maparachichi na apple zinazotosha kutengeneza kiasi cha juisi yako.
Osha vizuri matunda yako kwa usalama wa afya yako kisha menya na ondoa mbegu.
Kata vipande vinavyoweza kusagika.

Weka kwenye sahani au bakuli kisha saga kwenye blenda ili upate mchanganyiko sahihi. Unaweza kuchanganya na asali vijiko vikubwa vya chakula viwili au vitatu na maziwa kidogo.
Weka kwenye friji ipate ubaridi kidogo.

FAIDA ZAKE KIAFYA:
Virutubisho vilivyomo ndani ya matunda haya vina uwezo mkubwa wa kupunguza cholesterol kwenye damu hivyo kupunguza uwezekano mkubwa wa mtumiaji wa juisi hii kupatwa na magonjwa ya arteri/kuziba kwa mishipa ya damu.

TU FOLLOW KATIKA MITANDAO YA KIJAMII